Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bi.Mwanaidi Ali Khamisi amesema harakati mbalimbali za Kimataifa na Kitaifa zimewezesha usawa wa Jinsia kwenye ajira na kwenye nafasi za uteuzi.
Ameyasema hayo kwenye Kongamano la wanawake Wilayani Same ambapo alisema kwasasa kumekuwa na mabadiliko chanya katika ajira na nafasi za uteuzo ambapo Wanawake wamekuwa wakipewa nafasi.
Alisema Serikali imesaini mikataba mbalimbali ya Kimataifa yenye lengo la kuhakikisha Wanawake wanaingia kwa winging kwenye nafasi za maamuzi.
Uwepo wa wagombea wa viti Maalum vya nafasi za ubunge na udiwani pamoja na kundi Maalum la wanawake kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa ni jitihada za Serikali kuongeza uwakilishi WA Wanawake kwenye nafasi za maamuzi.
Akizungumza kwenye Kongamano hilo,Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni alisema Ofisi yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri wameona umuhimu wa kuwaleta Wanawake wa Same pamoja ili waweze kubadlishana mawazo katika kukuza Uchumi.
'Lengo la kongamano hili ni kuwaleta pamoja wanawake ilikujadili fursa za kiuchumi na kuwapa elimu ya kutumia nishati Safi ya kupikia ili kutunza mazingira "alisema Mhe.Kasilda
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mheshimiwa Yusto Mapande aliwataka wanawake kutambua kuwa wao sio washindani wa wanaume.
"Naunga mkono harakati za kumkomboa mwanamke dhidi ya unyanyasaji lakini niseme kuwa wanawake sio washindani wa wanaume bali kila mmoja atimize majukumu yake"alisema Mhe.Yusto
Katika Kongamano hilo lililojumuisha wanawake zaidi ya 400 kutoka maeneo mbalimbali ya Same na nje ya Same, mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo Utunzaji wa Mazingira,Afya,Fursa za Uchumi,Kuzuia ukatili wa kijinsia na Elimu ya Uongozi.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.