Halmashauri ya Wilaya ya Same imetumia Shilingi Bilioni 14 kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo kati ya fedha hizo bil 2.4 zilikuja nje ya ukomo wa bajeti..
Hayo yamebainishwa kwenye taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama kwenye Baraza la Madiwani la mwaka unaoishia Juni 30, 2024.
Katika taarifa yake iliyowasilishwa na Afisa Mipango Msaidizi Bw. Elisha Kapama ilibainisha kuwa fedha hizo zilitumika kujenga na kukarabati Miradi ya Elimu, Afya , Ujenzi wa ofisi za Kata na Vijiji na Miradi ya umwagiliaji.
Baadhi ya Miradi ya Elimu Sekondari iliyotekelezwa ni Ujenzi wa Shule mpya mbili za Sekondari za Malindi na Misufini Goma na mwingine ni Miradi ya Ujenzi wa nyumba tatu za walimu (2 in 1) kwenye shule za Sekondari Misufini Goma,Angella Kairuki na Malindi,miradi mingine ni umaliziaji wa mabweni kwenye shule nane za sekondari na unaliziaji wa bwalo.
"Kwa upande wa Afya Miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa vituo vya Afyakwenye Kata za Mtii, Ruvu na Myamba, umaliziaji na ukarabati wa zahanati nne za Masandare,Mwembe ,Duma na Kankokoro, ujenzi wa nyumba ya mtumishi zahanati ya Myamba na ununuzi wa vifaa tiba kwenye zahanati tano za Kirongwe,kalung'oyo,Kidunda, Kankokoro na Mgando pamoja na vituo vya Afya vitano vya Myamba, Mtii, Hedaru,Ruvu na Kisiwani' alisema
Kwa upande wa elimu Msingi Miradi iliyotekelezwa ni Ujenzi wa madarasa mapya zaidi ya 40 ,matundu ya vyoo 114 na ununuzi wa madawati 1,295 na ujenzi wa nyumba nne za walimu pamoja na ukarabati wa nyumba mbili za walimu.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mheshimiwa Yusto Mapande ameshauri Halmashauri kuhakikisha kuwa Miradi viporo inapewa kipaumbele cha umaliziaji wakati Serikali inapoanza mwaka mpya wa fedha 2024/2025.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.