Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mheshimiwa Yusto Mapande amesema kuwa Halmashauri hiyo imetenga bajeti kwaajili ya kuwezesha Kata zote za maeneo ya milimani kupata miche za parachichi zinazokomaa muda mrefu.
Ameyasema hayo wakati wa utoaji wa Tuzo za Mazingira za Shengena Environmental Award 2024 ambapo alisema lengo la Halmashauri ni kuhakikisha kuwa pamoja na kutunza Mazingira lakini pia wananchi waongeze kipato kupitia utunzaji wa Mazingira.
"Nilipongeze sana Shirika la Hope for Tanzania kwa kuanzisha Tuzo hii ambayo ni chachu katika kuhamasisha utunzaji wa Mazingira,Sisi kama Halmashauri tunaunga mkono juhudi hizi na tutatoa miche ya parachichi bure"alisema Mhe.Mapande.
Akizungumza katika hafla hiyo Meneja wa Shirika la Hope for Tanzania, Mchungaji Elisa Mrutu alisema Shirika hilo limeanzisha Tuzo hiyo ili kuhamasisha utunzaji wa Mazingira ambao unaambatana na kuinua uchumi wa wananchi.
"Na Mimi napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru benki ya Uchumi kwa kudhamini shughuli mbalimbali za Mazingira kwenye Wilaya ya Same "alisema Mch.Mrutu.
Kwa mwaka 2024 Kikundi cha Mazingira cha Juhudi Group (Kata ya Suji) kimefanikiwa kupata Tuzo hiyo kwa upande wa vikundi ambapo kwa watu binafsi Tuzo hiyo imechukuliwa na Kisimbo Farm(Kata ya Kisiwani) na Benki ya Uchumi imepata Tuzo kwa kudhamini shughuli za Mazingira.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.