Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amezitaka taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali kuhakikisha kwamba miti yote inayooteshwa kipindi hiki cha mvua inastawi.
Ameyasema hayo wakati akizindua zoezi la upandaji miti kwenye Wilaya ya Same kwa msimu wa 2023/24 ambapo alisema ni vema miti yote inayooteshwa ikasimamiwa vema iweze kuota na kukua.
“Tunaotesha miti mingi sana kila mwaka lakini tujiulize katika miti tunayootesha ni mingapi inayostawi na kukua vizuri,katika eneo hili tunapaswa kuwa makini” alisema Mheshimiwa Kasilda
Mkuu huyo wa Wilaya alisema mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na uharibifu wa mazingira ni makubwa mno kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu ambazo zinasababisha mitiu mingi kukatwa hivyo hatuna budi kukabiliana na hili kwa kuotesha miti kwa wingi na kuhakikisha miti hiyo inakua.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anastazia Tutuba alisema kwa upande wa taasisi za Serikali miti yote inayooteshwa inasimamiwa vema ambapo Zaidi ya asilimia 95 ya miti inayooteshwa hukua vema.
“Kila mwaka tunalengo la kuotesha miti mil.1.5 ambapo miti hugawanywa kwenye taasisi za serikali,taasisi binafsi na kwa mtu mmojammoja kwaajili ya kuotesha na imeshaanza kuleta tija” alisema Bi.Anastazia.
Alisema katika maeneo ya shule zote za Msingi na Sekondari zikiwemo za Serikali na binafsi zimezungukwa na miti mingi na bado wanaendelea kupewa miti ili waweze kuotesha.
Katika Uzinduzi huo jumla ya miti 1,000 ilioteshwa katika eneo linalozunguka Hospitali mpya ya Wilaya ya Same ambapo miti mingine 99,000 iligawanywa kwaajili ya kuoteshwa kwenye taasisi nyingine za serikali.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Tanzania Footmark Safaris ambao ndio waliofadhili miti hiyo Bi.Rehema Mghamba alisema wamekuwa wakishirikiana na Serikali kuotesha miti ili kuendeleza vivutio vya utalii.
“Sisi tunafanya biashara ya Utalii na unapozungumzia utalii kwa kiasi kikubwa tunamaanisha uwepo wa wanyama na viumbe hai vingine, sasa ili hivi vyote viwepo ni lazima tuendelee kuotesha miti tena kwa wingi”alisema Bi.Rehema.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.