• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Same District Council
Same District Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Same

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idaraya Elimu Sekondari
      • Rasili Mali Watu na Utawala
      • Ardhi Maliasili na Utalii
      • Fedha Na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Kazi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi.
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo Cha TEHAMA
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo Cha Uchaguzi
      • Kitengo Cha Manunuzi
      • Kitengo Cha Sheria
    • Kata
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
      • TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Stoo Ya Picha

"Elimu ni ufunguo wa maisha,wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa"-Mwenge wa Uhuru,Same DC.

Posted on: October 2nd, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Stacki Senyamule ameongoza maelfu ya wananchi wa Same katika zoezi la kupokea Mwenge wa Uhuru leo  Octoba  02,2018 kutoka Wilaya ya Mwanga uliokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Mwanga chini ya uangalizi wa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu,Charles Francis Kabeho.

Mapokezi ya Mwenge wa uhuru yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Njoro vilivyopo ndani ya kata ya Njoro.

Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mwenge wa Uhuru 2018 umetembelea jumla ya miradi saba yenye thamani ya Shil.1,304,058,700/=.Miradi hiyo ni pamoja na nyumba za watumishi walimu  zilizopo ndani ya kata ya Vumari uliogharimu Shil.147,076,200/=, mradi wa ofisi za shirika la mazingira la SMECAO zilizopo kata ya Kisima uliogharimu Shil.550,000,000/=.,mradi wa miundombinu ya maji uliopo ndani ya kata ya Kisima uliogharimu Shil.105,900,000/=,mradi wa kituo cha afya Ndungu uliopo kata ya Ndungu uliogharimu Shil.400,000,000/=.

Akizungumza wakati alipotembelea mradi wa nyumba za walimu  kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu Kabeho amekiri kuwa mradi huo ni mzuri na kwa kuwa walimu watakaokaa katika nyumba hizo watakuwa na motisha ya kazi na kupunguza gharama za maisha kuwa kubwa ambapo itapelekea kufanya kazi vizuri na kuongeza ufaulu wa wanafunzi. Pia elimu itolewe kwa wananchi wa Same ili wahamasike kushiriki katika kuwajengea walimu nyumba nyingi zaidi ili watoto wapate elimu.

Sambamba na hayo Mwenge wa Uhuru umezindua klabu 21 za kupinga rushwa zinazohusu vijana wa bodaboda zilizopo ndani ya kata ya Same zinazoundwa na jumla ya watu 410 wa Same mjini ambapo kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu Kabeho amezindua club hizo na kupanda mti pamoja na kuwakabidhi vyeti vijana hao.

Vijana hao walienda mbali zaidi wakionyesha kuelewa wanachokizungumza kwa kujibu maswali yote yahusuyo rushwa kutoka kwa ndugu Kabeho,huku wakitoa misemo mbalimbali na kuitikia,”Rushwa ni adui wa haki”na “Kataa rushwa, jenga Tanzania”

Mhe. Senyamule ameitaka klabu hiyo kuwa chachu ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii za Same na kuahidi kuwa pamoja nao katika kuhakikisha kilichoanzishwa kinakuwa kwa mafanikio na malengo yaliyokusudiwa yanatimia. Hii ni sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya Mhe.John Pombe Magufuli inayopinga na kupambana vikali dhidi ya rushwa za aina zote nchini.

Aidha,Baada ya taarifa ya Wilaya na miradi iliyotembelewa,kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru Mhe.Senyamule amemkabidhi Mwenge huo wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Elisha Mngwira ili aukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mhe.Mkuu wa mkoa wa Tanga na kuanza mbio za Mwenge 2018 ndani ya mkoa wa Tanga.

Ndugu Kabeho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akizindua nyumba za walimu kata ya Vumari shule ya Sekondari Vumari

Ndugu Kabeho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akizindua club za wapinga rushwa,kuwatunuku vyeti na kupanda mti katika kijiwe cha bodaboda.





Ndugu Kabeho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akimtwisha mwananchi ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa miundombinu wa maji Same mjini

Ndugu Kabeho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akitembelea kazi na vitu vinavotengenezwa na wanafunzi wa chuo cha ufundi cha Mtakatifu Joseph


Ndugu Kabeho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akiangalia samaki wanaofugwa katika bwawa la samaki kisiwani ambapo ni moja ya mradi aliouzindua



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 31, 2021
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI May 06, 2025
  • Siku ya kufanya usafi mwezi Septemba September 08, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2020 August 21, 2020
  • Tazama Vyote

Habari Za Sasa

  • WACHIMBA MADINI SAME WATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA

    May 19, 2025
  • SAME YAPANIA KUONGEZA UZALISHAJI WA MKONGE

    May 05, 2025
  • SAME YAPANIA KUONGEZA UZALISHAJI WA MKONGE

    May 05, 2025
  • SAME YAOMBA WIZARA YA KILIMO KUIPATAIA MICHE YA PARACHICHI

    May 01, 2025
  • Tazama Vyote

Video

KARIBU MWENGE WA UHURU SAME KILIMANJARO 2022
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Forms And Templates
  • Galleys
  • News
  • Events
  • Strategic Plan
  • Reports
  • Acts
  • Malalamiko

Viunganishi Vyenye Uhusiano

  • PO-Ralg
  • PO-Psm
  • e-Government Agency
  • Kilimanjaro Region
  • Employment
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Watembeleaji

free HitCounter

Ramani Ya Wilaya

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.