Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameelekeza Wizara ya Maji kuhakikisha kuwa ifikapo mwezi Juni ,2024 Mradi mkubwa wa Maji wa Same- Mwanga - Korogwe uwe umekamilika na kuanza kutoa huduma.
Ametoa agizo hilo Machi 21,2024 akiongea na wananchi wa Wilaya ya Same wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa ambapo alisema Mradi huo ukikamilika utakuwa suluhisho la changamoto ya upatikanaji maji kwa wananchi wa Wilaya za Same,Mwanga na Korogwe.
Mradi huo wenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Bilioni 300 umefikia asilimia 85.7 ya utekelezaji wake.
Mhe. Mpango amemtaka Waziri wa Maji Jumaa Aweso kusimamia kwa karibu wakandaraai wa mradi huo na kutatua changamoto zote zinazojitokeza katika utekelezaji ili kuhakikisha ifikapo Juni,2024 mradi huo uanze kutoa huduma ya maji.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.