• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Same District Council
Same District Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Same

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idaraya Elimu Sekondari
      • Rasili Mali Watu na Utawala
      • Ardhi Maliasili na Utalii
      • Fedha Na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Kazi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi.
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo Cha TEHAMA
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo Cha Uchaguzi
      • Kitengo Cha Manunuzi
      • Kitengo Cha Sheria
    • Kata
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
      • TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Stoo Ya Picha

DKT.MAHERA AAHIDI SERIKALI KUTOA FEDHA KUMALIZIA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA

Posted on: November 3rd, 2023

Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Wilson Mahera ameahidi kuipatia Wilaya ya Same magari  matatu ya Idara ya Afya ili kurahisisha kazi mbalimbali zinazofanywa na Idara hiyo katika Wilaya ya Same.

Dkt.Mahera ameyasema hayo akiwa katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa hospitali mpya ya Wilaya ya Same ambapo alisema magari yatakayotolewa kuwa ni magari mawili ya kubebea wagonjwa (ambulance)  pamoja na gari moja ya matumizi ya kawaida (hardtop).

"Utaratibu wa kupatiwa gari mbili yaani ambulance moja na hardtop moja umeshakamilika na mtazipokea wakati wowote lakini ambulance moja mtasubiri kidogo"alisema Dkt.Mahera

Pia Naibu Katibu Mkuu huyo ameahidi kuiongezea Hospitali hiyo fedha kwaajili ya kumalizia awamu ya pili ya mradi huo ambayo inajumuisha ujenzi wa Jengo la Utawala,Jengo la Kufulia,Wodi za Wagonjwa .

“Niwapongeze kwa kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali hii lakini niwaahidi kuwa tutaleta fedha za ukamilishaji wa Mradi huu ili majengo yote yaweze kutoa huduma na Mradi huu uweze kuwa na tija kwa wananchi” alisema.

Akitoa taarifa ya Ujenzi huo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same  Dkt. Alex Alexander alimuomba Naibu Katibu Mkuu kuipatia Hospitali hiyo pamoja na Wilaya nyongeza ya Watumishi kwani Wilaya inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wa Afya.

Aidha Dkt. Alex aliiomba Serikali kusaidia kujenga nyumba za Watumishi kwenye hospitali hiyo ya Wilaya kwani hakuna nyumba za kupanga karibu na eneo la Hospitali.

"Tunakabiliwa pia na changamoto ya ukosefu wa uzio kwaajili ya usalama kwasababu hapa ni mapitio ya Tembo hivyo tunahitaji uzio kwaajili ya usalama wa Watumishi na Wagonjwa”alisema Dkt Alex.

Naibu Katibu Mkuu Dkt Mahera alisema Serikali inatarajia kuajiri watumishi wapya wa sekta ya Afya mwezi huu (Novemba 2023) hivyo Wilaya ya Same itapata mgawo.

 Aidha Dkt. Mahera alisema katika kukabiliana na Upungufu mkubwa wa watumishi wa Afya hapa nchini Serikali inatarajia  kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambao ni wahitimu wa kidato cha nne ambao watapatiwa mafunzo ya miezi sita ili waweze kusaidia kutoa huduma za afya kwa kushirikiana na madaktari na wauguzi waliopo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 31, 2021
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI May 06, 2025
  • Siku ya kufanya usafi mwezi Septemba September 08, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2020 August 21, 2020
  • Tazama Vyote

Habari Za Sasa

  • MRADI WA SWASH ULIVYONUFAISHA WILAYA YA SAME

    April 03, 2025
  • WANANCHI WA MAKEI,SAME WAONDOKANA NA ADHA YA MAJI

    March 23, 2025
  • SAME YATOA ELIMU YA TAHADHARI YA MPOX MASHULENI

    March 18, 2025
  • MAAFISA UTUMISHI SIMAMIENI STAHIKI ZA WATUMISHI-DC SAME

    March 13, 2025
  • Tazama Vyote

Video

KARIBU MWENGE WA UHURU SAME KILIMANJARO 2022
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Forms And Templates
  • Galleys
  • News
  • Events
  • Strategic Plan
  • Reports
  • Acts
  • Malalamiko

Viunganishi Vyenye Uhusiano

  • PO-Ralg
  • PO-Psm
  • e-Government Agency
  • Kilimanjaro Region
  • Employment
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Watembeleaji

free HitCounter

Ramani Ya Wilaya

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.