Katika ziara yake ya kikazi Wilayani Same Tarehe 10/07/2019 Dkt.Bashiru Ally Katibu Mkuu CCM Taifa awataka wana CCM na watanzania wote kuilinda amani na utulivu wa nchi yetu.Asisitiza wanachama kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
Afurahishwa na kazi zinazofanywa na serikali na chama Wilaya ya Same.Akiri taarifa ya DC Same yamfilisi kwani imesema yote ya kutekeleza maelekezo yote ya serikali.Awataka wengine kuiga.
Aridhishwa na maendeleo ya mradi mkubwa wa maji(Same Mwanga).Aagiza kuhakikisha unaisha kwa wakati ili ilani ya CCM iwezeshe wananchi wa Same kuondokana na shida ya maji.
Ampongeza Waziri Mkuu mstaafu Mhe.John Malechela aliyealikwa kushiriki ziara hiyo pamoja na wananchi wa Same kwa kuijenga CCM na kuifanya salama mpaka sasa.
Asisitiza umuhimu wa CCM kuendelea kushika dola ni lazima.Ataka tuwaache wanaolialia badala ya kujenga chama chao kwani wameishiwa sera.Aaagiza wana CCM kuimarisha chama na kuhakikisha tunajitegemea badala ya kutegemea wafadhili kama vinavyofanya vyama vingine.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Ndg.Isaya Mngulu amuomba kurudi tena Same ili ajionee maeneo ya milima na ukubwa wa wilaya ya Same.
Mbunge wa Taifa Mhe.Anna Kilango amweleza ukubwa wa wilaya ya Same na kumuomba igawanywe kuongeza ufanisi na urahisi wa kuwafikia wananchi.
Mbunge David Mathayo aeleza tatizo la Tembo kuingia maeneo ya wananchi na ugumu wa barabara za Same.
Wanachama na wapenzi wa CCM wafurika na wampa kuwa kiongozi wa mila wa wapare na wamasai(Mfumwa na Aleigwanani).
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.