Katika kikao cha wadau wa maendeleo cha kupendekeza mpango wa 2021-2025 wa Wilaya ya Same,ambapo zaidi ya wacharo 100 walishiriki,Madiwani,taasisi za dini.
Walikubaliana kufanya mambo makubwa yatakayoifanya Wilaya ya Same kuwa kati ya zenye maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali kwa miaka 5 kwa kuungana na juhudi za serikali zinazoongozwa na Rais Mhe.Dr John Pombe Magufuli.
Katika kukamilisha kazi hiyo iliundwa timu ya watu 20 ili kuuweka mpango huo kitaalamu,kazi itakayokamilika tarehe 30/01/2020.
Kuanzisha kamati za kisekta zitakazosimamia utekelezaji wa mpango huo.
Kuainisha kazi zitakazofanywa na serikali,wadau wa maendeleo,wacharo na wananchi.
Kuwa na data kanza ya wacharo kwa uwezo wao wa kitaaluma,kimtandao na kirasilimali ili kujua nani atafanya nini.
Na kwa kuwa Wilaya ya Same ina upungufu mkubwa wa madarasa.Kikao kilikubaliana kila mcharo achangie fedha kuanzia Tshs.100,000/= na kuendelea kusaidia ujenzi wa madarasa ya Sekondari kabla ya tarehe 30/01/2021.
Tutatoa draft ya mpango kuanzia tarehe 01/02/2021.Ili tuweze kuupitia tena kabla ya kukamilisha na kuuchapisha kwa utekelezaji.
Kwa aliye tayari kutuma mchango wa madarasa atume kwa
Jina la akaunti:Same DC,Miscellaneous Deposit Account.
Namba ya akaunti: 40510000697
Benki:NMB Same branch
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.