Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija aamua kuwajibika mwenyewe kukusanya mapato ya ushuru wa ng'ombe katika mnada wa Ruvu Kombo Kata ya Ruvu baada ya mtendaji husika kushindwa kutimiza wajibu wake.Hii ni katika kuhakikisha mapato ya serikali hayapotei kwani kila ng'ombe analipiwa kiasi cha shilingi 5,000/= ambapo Bi.Anna-Claire Shija alikusanya mapato kwa ng'ombe 62 na kupata kiasi cha fedha taslimu shilingi 310,000/=
Akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji diwani wa kata ya Ruvu Mhe.Kiboko amesema mapato ya serikali yanapaswa kukusanywa na kusimamiwa kwa umakini ili kupata fedha za kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmamashauri.
Aidha Bi.Anna-Claire Shija aahidi kumchukulia hatua kali za kinidhamu mtendaji huyo kwa kushindwa kutimiza wajibu wake.Vile vile Bi.Anna-Claire ametoa wito kwa watumishi wengine wa halmashauri ya wilaya ya Same kutimiza majukumu,wajibu wao na kufanya kazi kwa bidii.
Bofya HAPA kusikiliza alichokisema Mkurugenzi Mtendaji.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.