Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija akagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa,vyoo matundu sita na bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Irikiponyi kijiji cha Ruvu Jiungeni kata ya Ruvu.Akizungumza na Mtendaji kata ya Ruvu,mjumbe wa kamati ya ujenzi,fundi kutoka idara ya ujenzi na fundi mkuu Bi.Anna-Claire Shija asisitiza majengo hayo kujengwa kwa kuzingatia ubora,viwango na muda uliowekwa mpaka kumalizika kwa ujenzi huo.
Aidha Bi.Anna-Claire Shija aipongeza jamii kwa kuchangia mawe na matofali katika majengo hayo.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.