Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija akagua mradi wa maji Rangeni(Rangeni weir intake) uliopo kata ya Hedaru ambapo mradi unagharimu kiasi cha fedha za kitanzania shilingi 299 milioni na unajengwa kwa fedha za serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mkandarasi aitwaye GTECH Solution Co.LTD,P.O.Box 60608 dsm.Wasimamizi wa mradi huu ni Halmashauri ya Same ikishirikiana na RS mkoa wa Kilimanjaro.
Mradi huu umelenga kuwapatia wananchi wa kijiji cha Hedaru(tambarare na mlimani) wapatao 18,476 huduma ya maji safi na salama ambapo umeshakamilika kwa asilimia 90% na tanki la kuchuja maji(coagution tank) limekamilika pamoja na ukuta mkubwa wa kukinga maji(weir).Mabomba yamelazwa na kufungwa kilometa 2.4 kuelekeza maji kwenye tanki lenye ujazo wa lita 150,000.
Mpaka sasa mkandarasi amelipwa shilingi milioni 172.
Aidha Bi.Shija amsisitiza mkandarasi kumalizia mradi huo mapema ili wananchi wa kijiji cha Hedaru wapate huduma ya maji safi na salama.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.