Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija akiwa ameambatana na wataalamu toka idara mbalimbali zenye miradi inayotarajiwa kufunguliwa na kuzinduliwa na Mwenge wa uhuru tarehe 2/10/2018 amekagua miradi hiyo ikiwemo mradi wa nyumba za walimu shule ya sekondari Vumari,jengo la SMECAO,mradi wa maji kata ya kisima,vyumba vya madarasa shule ya msingi Ijinyu,kisima cha maji kilichopo Maore na mradi wa bwawa la samaki aina ya kambale.
Wataalamu toka idara mbalimbali washauri maboresho mbalimbali katika miradi hiyo ikiwemo mradi wa maji kata ya kisima kuboreshwa zaidi na jengo la SMECAO kumalizwa kwa haraka ili kumalizika kabla ya tarehe ya Mwenge wa uhuru kufika.
Aidha Bi.Anna-Claire Shija asisitiza miradi hiyo kuboreshwa kwa viwango na kwa umakini ili kukidhi vigezo.
Nyumba za watumishi waalimu shule ya sekondari Vumari kama inavyoonekana hapo chini
Jengo la SMECAO kama linavyoonekana hapa chini kwa muonekano wa ndani
Mradi wa maji kata ya Kisima kama inavyoonekana hapo chini
Mradi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Ijinyu kama inavyoonekana hapo chini
Mradi wa bwawa la samaki aina ya kambale kama unavyoonekana hapo chini
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.