Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same ametoa zawadi na vyeti kwa wanafunzi na Walimu waliowezesha Timu za UMISETA na UMITASHUMTA kufanya vizuri katika mashindano ya michezo kuanzia ngazi ya Wilaya ,Mkoa hadi Taifa.
Akitoa zawadi kwa walimu na wanafunzi hao , Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Same Bi. Anastazia Tutuba alisema zawadi hiyo ni motisha tu kwa walimu na wanafunzi walioiwakilisha vema wilaya ya Same.
"Wakati wanaondoka kwenda kwenye mashindano niliwaambia waende wakang'ae huko na kweli wamefanya hivo napenda kuwapa zawadi hii ya shilingi laki tano ili wakati mwingine wajitahidi zaidi na kupeperusha bendera ya Same vizuri" alisema Bi.Anastazia
Mkurugenzi huyo alisema kwa kuanzia ameamua kutoa kiasi hicho cha fedha lakini wakati mwingine Halmashauri itajipanga ili iweze kuwapongeza kwa kikubwa zaidi.
Akizungumzia mafanikio ya Timu za Wilaya ya Same katika Mashindano hayo, Kaimu Afisa Utamaduni,Sanaa na Michezo wa Wilaya ya Same Bw.Nevlin Nyange alisema kwa ngazi ya Mkoa katika michezo wa mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana zilishika nafasi ya kwanza, mchezo wa wavu ilishika nafasi ya kwanza kwa wasichana na mchezo wa kikapu nafasi ya pili kwa wavulana.
Amesema mchango wa Wilaya ya Same katika kuunda timu ya Mkoa imetoa wanafunzi 29 na waalimu 2 kwa michezo ya umitashumta na umisenta ambayo ni sawa na asilimia 34.8 katika timu ya Mkoa.
"Mkoa wa Kilimanjaro umeshika nafasi ya nne kwa Tanzania bara na Visiwani na kutoa mwalimu mmoja wa kike kwa mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Rwanda hii ni hatua kubwa kwa Mkoa na Wilaya yetu ya Same" amesema
Mkoa wa Kilimanjaro kwa mashindano ya mwaka uliopita 2022 ulishika nafasi ya 6 kitaifa huku kwa mwaka huu 2023 ukishika nafasi ya 4 kitaifa ambapo Same inajivunia kuwa sehemu ya mafanikio haya ya Mkoa.
Bw.Nevlin alisema kwa sasa Wilaya inaendelea kunoa timu zake kwaajili ya maandalizi ya mwakani ili kuusaidia Mkoa kuiendea nafasi ya pili kama sio ya kwanza Kitaifa.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.