Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama amewatakia kheri wanafunzi wa Kidato cha Sita 2024 ambao wameanza mitihani yao.
Jumla ya wahitimu 814 wanafanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha Sita mwaka huu ambapo wanafunzi 795 wapo kwenye Shule mbalimbali za Sekondari na 19 ni watahiniwa wa kujitegemea.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Same Bi.Neema Lemunge amesema maandalizi yote muhimu kwaajili ya mitihani hiyo yamekamilika.
"Maandalizi yote yamekamilika na mitihani imeshaanza kwenye vituo vyetu 09 ambapo 03 kati ya hivyo ni vya Serikali na 06 vya binafsi "alisema Bi.Lemunge.
Wanafunzi waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo wasichana ni 163 na wavulana ni 632 na kwa upande wa watahiniwa binafsi wanawake ni 08 na wanaume ni 11.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.