Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.James Mhagama amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri hiyo shilingi bil 3.9 kwaajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali kwenye sekta ya Elimu Sekondari kwa mwaka 2023/2024.
Bw.Mhagama alisema kuwa fedha hizo zinatekeleza miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa shule za Sekondari Wilayani humo ambapo alisema miradi hiyo ni pamoja na umaliziaji wa Mabweni sita kwenye shule za Sekondari Bangalala,Kwizu,Madiveni,Makanya,Kibacha,Bombo Kimala na ujenzi wa mabweni mawili kwenye shule kongwe ya Sekondari Same na shule mpya ya Misufini Goma.
Alisema Halmashauri pia imepokea fedha kwaajili ya ujenzi wa shule mpya za Sekondari ambazo ni Malindi, Angellah Kairuki, Hedaru,Misufini Goma ambapo shule mbili zimeshapokea wanafunzi na shule mbili zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
“Tumepokea pia fedha za kujenga nyumba tatu za watumishi ambazo ni 2 in 1 kwenye shule za Sekondari Misufuni Goma,Angellah Kairuki, na Malindi na ujenzi wake upo kwenye hatua za awali” alisema Bw.Mhagama
Alisema fedha hizo pia zitatumika kujenga Madarasa mapya 22 na matundu ya vyoo 72 kwenye shule mbalimbali za Sekondari Wilayani humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Yusto Mapande alimshukuru pia Rais Samia kwa fedha hizo ambazo zimepokelewa kwenye Halmashauri na kuahidi kuwa Miradi yote itakamilika kwa wakati na kwa ubora.
“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutupatia fedha hizi na tunachoweza kumuahidi ni kwamba miradi yote itakuwa na ubora unaotakiwa” alisema Mheshimiwa Mapande.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.