Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija akagua mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa,bweni na vyoo katika shule ya sekondari Irikiponi kata ya Ruvu ambapo amebaini dosari katika vyumba vya madarasa na vyoo huku fundi mkuu katika ujenzi huo akijaribu kumshawishi kwamba amekamilisha kazi lakini uhalisia ni kwamba kazi imefanyika chini ya viwango.Bi.Shija amemtaka fundi huyo kukamilisha kazi kwa ubora unaotakiwa kwa maana ya kuzifanyia kazi dosari zote alizoziona ikiwa ni pamoja na kubadilisha rangi ya njano kwani sio rafiki kwa mwanafunzi kwa mazingira ya kujifunzia.
Aidha Bi.Anna-Claire Shija amemwagiza Mhandisi wa ujenzi kumsimamia fundi huyo arudie kazi kwa viwango vinavyohitajika ndipo akabidhiwe mradi huo.
Hapo chini ni muonekano wa vyumba vya madarasa
Ufuatao hapo chini ni muonekano wa vyoo kwa ndani na nje
Muonekano wa ndani wa bweni ambalo bado halijakamilika
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.