Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amewataka wananchi kutumia vyema uwepo wa madaktari bingwa wa Dkt.Samia ambao wapo Hospitali ya Mji-Same kwa muda wa siku saba kuanzia Oktoba 21-27, 2024.
Ametoa wito huo wakati akipokea madaktari hao ambapo alisema matibabu yote yatatolewa kwa gharama nafuu na za kawaida za kila siku zinazotumika kwenye Hospitali ya Mji Same, bima za afya NHIF na ICHF pia zitatumika.
Huduma zinakazotolewa ni matibabu ya kibingwa ya wanawake na ukunga, watoto na watoto wachanga, upasuaji au mfumo wa mkojo, usingizi na ganzi, magonjwa ya ndani, kinywa na meno, pamoja na tiba ya mifupa na magonjwa ya ndani.
"Matibabu yote yatatolewa kwa gharama nafuu na za kawaida za kila siku zinazotumika kwenye Hospitali hiyo, bima za afya NHIF na ICHF pia zitatumika pamoja na kulipa kwa fedha tasilimu (cash)" alisema Mkuu wa Wilaya.
Mheshimiwa Kasilda ameshukuru jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuisogezea Wilaya ya Same huduma za kibingwa.
Madaktari bingwa wa Dkt. Samia awamu ya pili wapatao sita (6) pamoja na muuguzi bingwa mmoja wamepokelewa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro ambao watakuwa na kambi ya siku saba kuanzia Oktoba 21 hadi 27 Hospitali ya Mji -Same kutoa huduma ya matibabu ya kibingwa.
Awamu ya kwanza ya kambi hizo za kibingwa Wilayani Same ilifanyika Mei 20 hadi 24 mwaka huu ambapo wananchi zaidi ya elfu nane (8,000) wenye magonjwa mbalimbali walihudumiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.