Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni ameitaka Kampuni ya BuildTech Engineering Co.Ltd iliyoshinda zabuni ya Mradi wa Tsh.Bil.1.05 wa kusambaza Maji kwenye vijiji vya mbakweni na Msindo kuhakikisha kuwa wanawapa ajira za muda vijana na wanawake wa eneo hilo.
Ameyasema hayo wakati wa kusaini mkataba wa Mradi huo na kutambulisha Mradi huo kwa wananchi wa Kata ya Msindo.
"Leo hapa tumeshuhudia utiaji saini wa Mkataba huu wenye thamani ya shilingi bilioni moja,tunategemea hii fedha aliyoileta Rais wetu Samia Suluhu Hassan anatarajia iwanufaishe pia wananchi wa hapa kwa kupewa kazi wanazoweza kufanya"alisema Mkuu huyo.
Amesema pamoja na Mradi huo kutarajiwa kuondoa shida ya Maji kwa wananchi zaidi ya elfu nne lakini pia fedha hizo tunatarajia zinufaishe pia vijana kwa kupata ajira ndogondogo.
Akitoa taarifa ya Mradi huo Meneja wa RUWASA Wilaya ya Same Bw.Abdallah Gendaheka alisema Mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Mei 31,2024.
"Niwaombe wananchi wa Kata ya Msindo mhakikishe kwamba mnakuwa walinzi wa vifaa vya Mradi huu,msiruhusu vifaa kuibiwa au kuharibiwa kwa njia yoyote"alisema Meneja huyo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Msindo Mheshimiwa Yusto Mapande aliishukuru Serikali kwa kuwapatia Mradi huo na kuahidi kuusimamia na kuutunza.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.