Wananchi wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wameungana na watanzania wengine katika kusherehekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ambao ulisababisha kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiswa April 26 mwaka 1964 na waliokuwa marais wa nchi hizi mbili ambao ni Hayati Julius Kambarage Nyerere wa Tanganyika na Hayati Abeid Aman Karume wa Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni aliongoza Maadhimisho haya WIlayani Same ambapo aliwapongeza viongozi wa Tanzania kutokana na busara na hekima zao zilizosababisha Muungano huu uendelee kudumu na wananchi hatuna budi kuendelea kuulinda Muungano.
Alisema miaka 60 ni mingi sana na watanzania tunapaswa kujipongeza na kuwapongeza viongozi wote walioliongoza Taifa hili tangu nchi hizi mbili zilipoungana.
Wilayani Same kilele cha sherehe hizo kimefanyika kwenye viwanja vya stendi ya mabasi ambapo Mkuu wa Wilaya alisema viongozi wote waliopita wameitendea mema nchi hii ambapo kwasasa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anaendeleza vema gurudumu hilo.
Mheshimiwa Kasilda alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya ya Same Miradi mbalimbali ambayo imewezesha uboreshaji mkubwa katika sekta za Afya, Elimu na Kilimo.
Alisema kuwa kabla ya Muungano Same kulikuwa na shule moja tu ya Sekondari lakini ndani ya miaka 60 kuna jumla ya Shule 66 sawa na ongezeko la shule 65 ambapo za Serikali ni 45 na binafsi 20, vile vile Shule za Msingi zilikuwa 14 lakini kufikia 2024 kumekuwa na ongezeko la Shule 192 miongoni mwao za Serikali ni 174 na binafsi ni 18 na kufanya kuwa na jumla ya Shule 206 zilizosajiliwa.
Kaulimbiu ya Muungano mwaka huu inasema “Miaka 60 ya Muungano Tumeshikamana na tumeimarika kwa maendeleo ya Taifa letu
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.