Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri Bw.Jimson Mhagama pamoja na maafisa ugani Wilayani humo kwa kuendelea kutoa elimu ya kilimo cha kisasa.
Mheshimiwa Kasilda ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Same kwenye maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini yanayofanyika kwenye viwanja vya Themi,Njiro Mkoani Arusha.
“Kwakweli nimefurahishwa sana kuona jinsi wakulima walivyoshirikishwa kwenye maonesho haya, lakini pia nimefurahishwa na vipando vya mazao mbalimbali yaliyopo hapa kwenye banda letu kwani mazao yamestawi vizuri sana” alisema
Mheshimiwa Kasilda alisema amefurahishwa pia na teknolojia mpya ya kutumia mikunde pori kurutubisha ardhi lakini pia kupunguza athari za wadudu waharibifu wa mazao.
“Niwashauri wataalam wangu ujuzi wowote wenye manufaa kwa wakulima na wafugaji wetu ambao mmeupata kwenye maonesho ya Nanenane mhakikishe mnaufikisha kwa wananchi wetu ili waweze kuboresha kilimo na ufugaji wao uweze kuwa na tija” alisema Mkuu huyo
Akizungumza kwa niaba ya wakulima waliowezeshwa kushiriki maonesho hayo,Mwenyekiti wa wakulima wa Tangawizi Mamba Myamba,Same Bw.Mbaruku Ally aliishukuru Serikali kwa kuwawezesha kushiriki maonesho hayo.
“Tunaishuku Serikali Wilayani Same kwa kuona umuhimu wa kuhakikisha tunashiriki maonesho haya,hii ni sehemu ambayo tunajifunza mambo mengi yanayotusaidia kuboresha kilimo na ufugaji”alishukuru Bw.Mbaruku
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.