DC Same Mhe.Rosemary Senyamule,ameungana na wadau kuchangia ujenzi wa msikiti wa Taqwa ili kukamilisha kazi ya kuezeka msikiti,kabla ya kuanza hatua nyingine za umaliziaji.Akikabidhi mchango huo DC Same alisema "Tutaendelea kushirikiana na taasisi za dini kwani ndizo zinachangia wananchi wetu kukaa kwa amani na utulivu,naamini utulivu huu unachangiwa na wananchi kuelewa masomo ya dini yanayohimiza amani.Anawataka wananchi kusherehekea sikukuu ya Eid kwa utulivu na amani.
Naye Shekh wa Wilaya akipokea mchango huo kwa niaba ya msikiti alishukuru na kuahidi kutumia fedha hiyo kama ilivyokusudiwa.Alishukuru serikali kwa kuwa karibu na viongozi wa dini,aahidi kuendeleza ushirikiano.
Aidha DC aishukuru Kampuni ya Badr East Africa kwa kushiriki katika mchango huo.
Eid Mubarak
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.