• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Same District Council
Same District Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Same

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idaraya Elimu Sekondari
      • Rasili Mali Watu na Utawala
      • Ardhi Maliasili na Utalii
      • Fedha Na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Kazi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi.
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo Cha TEHAMA
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo Cha Uchaguzi
      • Kitengo Cha Manunuzi
      • Kitengo Cha Sheria
    • Kata
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
      • TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Stoo Ya Picha

DC KASILDA AZITAKA TAASISI YA SERIKALI KUJIIMARISHA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO

Posted on: February 6th, 2025


Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, amezitaka taasisi za serikali zinazokusanya mapato kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi ndani ya kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuimarisha uwezo wao wa kifedha na kufanikisha malengo ya ukusanyaji wa mapato waliyojiwekea.

Taasisi hizo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mamlaka ya Maji Same Mwanga (SAMWASA), Hifadhi ya Taifa Mkomazi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Halmashauri ya Wilaya ya Same pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Akizungumza katika kikao cha mapato ambacho kimewakutanisha Halmashauri ya Wilaya ya Same, wakuu wa taasisi za serikali ndani ya wilaya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni amesisitiza umuhimu wa kuboresha vyanzo vya mapato vilivyopo na kuanzisha vipya ili kuhakikisha taasisi zinakusanya mapato kwa asilimia 100 au zaidi kwa mwezi na kwa mwaka.

"Ni lazima tuwe wabunifu katika kubuni vyanzo vipya vya mapato ili tuweze kufanikisha malengo yetu ya ukusanyaji wa mapato. Bila kuboresha vyanzo hivi, taasisi zetu zitashindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato," alisema Mhe. Kasilda.

Katika kikao hicho, ilibainika kuwa moja ya changamoto zinazoathiri ukusanyaji wa mapato ni uharibifu wa miundombinu unaofanywa na baadhi ya wananchi wasio waaminifu, hususan katika sekta ya usambazaji maji. Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya amesema msimamo wa serikali ni kuwachukulia hatua kali wote watakaobainika kuharibu miundombinu hiyo kwa kuwa vitendo hivyo vinakwamisha maendeleo.

"Serikali haitavumilia vitendo vya uharibifu wa miundombinu vinavyofanywa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi. Tutahakikisha wote wanaobainika wanachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa sababu hii miradi ni kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wenyewe kupata huduma karibu" amesisitiza Mhe.  Kasilda.

Lengo la kikao hicho ni Kupitia na kufanya tathmini ya makusanyo ya mapato ya ndani kwa kila taasisi, kubaini changamoto za ukusanyaji wa mapato na kuzitafutia suluhisho pamoja na kupanga mikakati ili kuhakikisha malengo yanatimia kwa asilimia 100 au zaidi.

Hatua hii inalenga kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato, kuhakikisha uwajibikaji, na kusaidia taasisi za serikali kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 31, 2021
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI May 06, 2025
  • Siku ya kufanya usafi mwezi Septemba September 08, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2020 August 21, 2020
  • Tazama Vyote

Habari Za Sasa

  • MRADI WA SWASH ULIVYONUFAISHA WILAYA YA SAME

    April 03, 2025
  • WANANCHI WA MAKEI,SAME WAONDOKANA NA ADHA YA MAJI

    March 23, 2025
  • SAME YATOA ELIMU YA TAHADHARI YA MPOX MASHULENI

    March 18, 2025
  • MAAFISA UTUMISHI SIMAMIENI STAHIKI ZA WATUMISHI-DC SAME

    March 13, 2025
  • Tazama Vyote

Video

KARIBU MWENGE WA UHURU SAME KILIMANJARO 2022
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Forms And Templates
  • Galleys
  • News
  • Events
  • Strategic Plan
  • Reports
  • Acts
  • Malalamiko

Viunganishi Vyenye Uhusiano

  • PO-Ralg
  • PO-Psm
  • e-Government Agency
  • Kilimanjaro Region
  • Employment
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Watembeleaji

free HitCounter

Ramani Ya Wilaya

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.