Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amezindua Msimu wa pili wa tasha la Same Utalii Festival (SUF) litakaloanza Desemba 20 hadi 22 mwaka huu 2024.
Tamasha hilo linalotarajia kuwa na wageni zaidi ya elfu ishirini litafanyika kwenye viwanja vya MYCA Same mjini.
Tamasha hilo litatanguliwa na SUF marathon(Utalii wa Afya) ambayo itakuwa na mbio za umbali wa Kilometa 5, 10 na 21 ili wananchi waweze kujiweka sawa kutembelea vivutio vya Utalii.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya amewakaribisha Wananchi wa ndani na nje ya Wilaya ya Same kushiriki Tamasha hilo.
Meneja wa SUF Bw.Hatibu Joshua amesema SUF Msimu wa pili itakuwa ya kihistoria kwani inatarajia kusafirisha watalii toka Dar es Salaam,Pwani na Tanga kwa njia ya treni.
"Treni tutakayotumia itakuwa na mabehewa manne ya SUF ambapo tutakuwa na behewa la Vinywaji,tutakuwa na behewa la nyama Choma,behewa la Music na behewa la Michezo ya watoto,tumejipanga vizuri"alisema Meneja huyo.
Alisema Utalii wa tre ni kutoka Dar es Salaam hadi Wilayani Same, safari itaanza Desemba 18 na kuwasili ni Desemba 19.
Tamasha la SUF litajumuisha pia Utalii kwenye hifadhi ya Taifa Mkomazi (nyumbani kwa faru weusi),kupanda Mlima Shengena na kupanda Mlima kidenge.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.