Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amewataka wasimamizi wasaidizi wa Uchanguzi wa Serikali za Mitaa ngazi ya Jimbo,Kata na Vijiji kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma wakati wote watakapokuwa wanasimamia Uchaguzi huo.
Mheshimiwa Kasilda ametoa angalizo hilo wakati akifungua mafunzo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wasidizi ngazi ya Kata na Vijiji ambapo alisema njia pekee ya kufanya kazi hiyo kwa uadilifu ni kwa kuzingatia miiko ya utumishi wa umma.
“Ukizingatia maadili ya utumishi wa Umma utaepuka rushwa,utafanya kazi kwa weledi na kujituma,utaweza kutunza siri za ofisi na utakuwa Mzalendo kwa Taifa lako” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha amewahimiza Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa zote sahihi kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kushiriki kikamilifu katika hatua zote zinazowahusu ikiwemo kujiandikisha kwenye Daftari la Mkazi ili waweze kuwa na sifa ya kupiga kura.
“Hakikisheni mnasoma miongozo yote ya uchaguzi na kuielewa ili muweze kutekeleza jukumu hili kwa weledi na pia zingatieni ratiba iliyotolewa ya Uchaguzi na muifuate ili msiwe mbele wala nyuma ya ratiba” alisema.
Akizungumza katika mafunzo hayo Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Same Mashariki na Same Magharibi Bw.Jimson Mhagama amewataka wasimamizi wasaidizi hao kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mafunzo hayo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi 134 ngazi ya Kata na Vijiji yalitanguliwa na kula kiapo cha uadilifu ambapo Hakimu Levina Masha aliwaapisha.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Hapa nchini unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu ambapo Oktoba 11 hadi 20 kutakuwa na zoezi la wapiga kura kujiandikisha kwenye Daftari la Mkazi ili waweze kuwa na sifa ya kupiga kura.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.