Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro imetoa vyeti vya pongezi kwa Taasisi ambazo zimefanya vizuri kwenye ukusanyaji wa Mapato Wilayani humo kwa kipindi cha Aprili hadi Juni 2024.
Taasisi hizo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao katika kipindi cha miezi mitatu wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni 871 makusanyo ambayo ni ongezeko la shilingi Milioni 193.5 ikilinganishwa na makusanyo ya wakati kama huo kwa mwaka wa fedha uliopita.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vyeti hivyo Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Kasilda Mgeni amepongeza jitihada mbalimbali zinazo fanywa na Taasisi hizo kwenye ukusanyaji wa Mapato, huku akisisitiza kuendelea kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii ili waweze kufanya vizuri zaidi.
Katika kuhakikisha kwamba mapato yanaongezeka Wilayani Same,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeanzishwa kikao maalumu cha kila mwezi cha kujadili mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ambacho kinalenga kushauriana namna ya kuweza kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato.
Pamoja na Mamla ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi nyingine zilizofanya vizuri ni Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.