Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amewakutanisha waendesha bodaboda Wilayani Same na taasisi za kifedha ili kuwaunganisha waweze kukopeshwa na kujiendeleza kiuchumi.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu huyo wa Wilaya alisema kazi hya kuendesha bodaboda kwa sasa inafanywa na watu wengi hivyo ni vema wakatambulika na kuweza kukopeshwa na mabenki.
“Leo nimewakutanisha hapa waendesha bodaboda na taasisi za kifedha ili muweze kukopeshwa na kujiendeleza kiuchumi na ninaamini kikao cha leo kitakuwa na tija kwa pande zote mbili” alisema
Mkuu wa Wilaya pia alipongeza viongozi wa Umoja wa waendesha bodaboda Wilayani Same kwa kufanikiwa kusajili kikundi na kukisajili jambo ambalo linasababisha taasisi za fedha kuwaamini na kuweza kuwakopesha.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Umoja huo Bw.Musa Hashim alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuasisi uanzishwaji na usajili wa Umoja huo ambao kwasasa una wanachama 124.
“Tunamshukuru sana Mkuu wetu wa Wilaya kwani tulipokutana nae kwa mara ya kwanza alitushauri kuunda umoja na kuusajili ili tuweze kupatiwa mikopo na taasisi za fedha na tayari tumeunda umoja” alisema Bw.Hashim
Kwa Upande wake Meneja wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) tawi la Same Bw. Mohamed Amri alisema kwasasa benki hiyo inaweza kuwakopesha kwa kupitia kikundi chao.
Nae Afisa Mahusiano wa benki ya NMB Same Bw.Mongi Kundael alisema Benki hiyo ni benki inayojali wajasiriamali na imejipanga kuweza kuwakopesha waendesha bodaboda hao.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.