Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Kasilda Mgeni amewataka wananchi na taasisi Wilayani humo kuzitumia vema mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuotesha miti ili kutunza mazingira.
Mhe.Kasilda ameyasema hayo wakati akiongoza zoezi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari Same ambapo zaidi ya miti 200 iliweza kuoteshwa.
Miti hiyo ilioteshwa na Mkuu wa Wilaya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Fedha ya Halmashauri ambao walikuwa katika Ziara ya kawaida ya kukagua Miradi ya Maendeleo.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Yusto Mapande pia iliotesha miti pia katika eneo inapojengwa Hospitali mpya ya Wilaya.
Akizungumza wakati wa kuotesha miti Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Yusto amezitaka Taasisi hizo kuhakikisha kuwa mti inayooteshwa inatunzwa vema ili isife.
"Hii miti tunayootesha hakikisheni kwamba haifi,muitunze kwa faida yetu na vizazi vijavyo"amesema Yusto
Akizungumzia uoteshaji wa miti Wilayani humo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bi.Anastazia Tutuba amesema tayari Wilaya hiyo imeshaotesha miti zaidi ya 900,000 kati ya miti mil. 1.5 inayotakiwa kuoteshwa kufikia June,2023.
"Tuna uhakika hadi kufikia mwezi June tutakuwa tumefikia lengo la kuotesha miti 1.5 tulilojiwekea"amesema Anastazia
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.