Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amewataka watumishi wa Afya Wilayani humo kufanya kazi wa kujituma na kuhakikisha kila mgonjwa anayehudumiwa anaridhishwa na huduma zinazotolewa.
Ametoa with huo wakati akifungua kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Wilaya,ambapo amesema Wilaya kuwa na watumishi wachache wa afya isiwe sababu ya wananchi kutopatiwa huduma bora.
"Niwapongeze sana kwani pamoja na uchache wenu lakini mnafanya kazi nzuri,endeleeni kujituma wakati Serikali ikiendelea kuajiri ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa watumishi"alisema Mkuu wa Wilaya.
Aidha amewataka Maafisa Afya na watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanafanya ukaguzi kwenye kila Kaya na watakapobaini hakuna vyoo hatua stahili zichukuliwe.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same Dkt.Alex Alexander amesema Kwa mwaka 2024 Idara ya Afya Wilayani humo ilifanikiwa kutoa huduma ya usafirishaji wa dharura Kwa kinamama wajawazito 326 na watoto 62 na kuwawezesha kufikia huduma za afya.
"Idara pia ilifanikiwa kufikia asilimia 100 ya ukusanyaji mapato lindwa ambapo Kwa upande wa Utekelezaji wa Mkataba wa Afya za lishe Wilaya imefanikiwa Kwa asilimia 97" amesema Dkt.Alex.
Kwa upande wa upimaji virusi vya UKIMWI na ushauri nasaha Wilaya ya Same Kwa mwaka 2024 ilipima watu 38,164 ambapo kati yao 532 waligundulika kuwa na maambukizi na wameanzishiwa dawa za kufubaza virusi ARV.
Dkt.Alex alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Kwa kunipatia Wilaya ya Same magari manne ya wagonjwa (Ambulance )ambazo zinatumika hospitali ya Wilaya,hospitali ya Mji na kwenye vituo vya Afya
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.