DC wa Same Mhe.Rosemary Senyamule akuta kata nzima haina hata kijiji kimoja, shule ilianguka tangu mwaka 2011 hadi leo yamejengwa madarasa mawili tu wanasubiri fedha za serikali. Awaonya kuwacheleweshea wananchi maendeleo kwani wananchi wanao utayari wanachokosa ni uhamasishaji kutoka kwa viongozi."Kukosa malengo, utayari na nia ya dhtati ya kuwatumikia wananchi kumetuchelewesha", alisema Mhe.Rosemary Senyamule.
Aaagiza kila kijiji kisichokuwa na zahanati kuanza ujenzi mwaka huu na kukamilisha mwaka 2019."Mtendaji asiyeweza kuhamasisha maendeleo, kazi ya utendaji imemshinda", alisema DC huyo.
Akagua jengo la zahanati lililofikia hatua za umaliziaji. Akagua eneo la kujenga ofisi ya kata ya Mtii.
Naye Afisa tarafa Chome-Suji ndugu Sixbert afanya msaragambo wa kusafisha eneo la kujenga zahanati ya kijiji cha Rikweni kata ya Tae. Mirungi yang'olewa kwa asilimia 90%.
Wilaya ina vijiji 100 na kati ya hivyo, vijiji 49 vina huduma za afya; bado vijiji 51 havina zahanati. Ambapo wilaya kwa kushirikiana na wananchi/ wadau wanataka kumaliza kazi hiyo ifikapo 2019.
Aidha Mhe,Rosemary Senyamule aagiza maafisa tarafa wote kila ifikapo jumatatu kushirikiana na wananchi kwenye za maendeleo.
Bofya HAPA kumsikiliza Mhe,DC akiwafunda viongozi wa kata na vijiji.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.