Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amelaani vikali mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sinangoa "A" Kata ya Ndungu Bw.Charles Mnguruto (58) ambaye aliuwawa na watu wasiojulikana kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali.
Akizungumza wakati wa maziko ya Mwenyekiti huyo Mkuu wa Wilaya aliagiza Jeshi la Polisi kufanya oparesheni maalum ya kuwasaka na kuwakamata haraka watu walioshiriki kupanga njama na kutekeleza maujai hayo ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Mwenyekiti huyo aliuawa April 26 mwaka huu akiwa kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi baada ya kuvamiwa na kushambuliwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali.
Aidha amewaonya wananchi kutolipiza kisasi na kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake waiachie Serikali kupitia vyombo vya usalama iweze kuwasaka na kuwachukulia hatua wahusika.
"Mimi na Kamati yangu ya Ulinzi na Usalama tumesikitishwa sana na mauaji haya ya kikatili ya Kiongozi wetu mwadilifu wa wa Serikali ambaye wananchi walimuamini na kumchagua kuongoza kwenye kitongoji hiki cha Sinangoa "A", niseme tu wananchi wangu matukio haya hayakubaliki na siyo sawa kabisa kutendeana"alionya Mkuu wa Wilaya.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.