Katibu Tawala wa Wilaya ya Same Bi.Upendo Wella leo ameongoza mamia ya Wananchi wa Same kufanya usafi na kuotesha miti kwenye chanzo cha Maji cha Water kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Katibu Tawala Bi. Wella aliwataka wananchi kujenga tabia ya kufanya usafi kwenye maeneo yote yanayowazunguka.
"Leo tumeadhimisha siku ya Uhuru Kwa kufanya usafi na kuotesha miti hivyo shughuli hizi ziwe endelevu" alisema
Aidha aliwataka wananchi kuendelea kulinda na kudumisha amani ambayo imeendelea kuwepo kwa miaka 63.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama aliwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kuadhimisha siku ya Uhuru.
"Mwitikio umekua mkubwa,wananchi wamejitokeza kwa wingi kufanya usafi na tumeotesha miti zaidi ya 100 kwenye chanzo cha Maji cha Water "alisema Mhagama
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.