Wilaya ya Same imekamilisha zoezi la chanjo dhidi ya kansa ya mlango wa kizazi kwa kwa mafanikio makubwa kwa kufikia asilimia 122 ya malengo tarajiwa.
Chanjo hiyo iliyokuwa inaendeshwa kitaifa kwa wasichana wenye umri wa miaka 9-14 ilianza kutolewa April 22-26 mwaka huu kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same Dkt. Alex Alexander amesema Wilaya ililenga kuchanja wasichana 3,768 lakini hadi kukamilika kwa zoezi hilo jumla ya wasichana 4,617 waliweza kufikiwa ambao ni sawa na asilimia 122.
Hata hivyo Dkt. Alex alisema kama kuna wasichana wenye sifa za kupata chanjo hiyo na wameikosa wafike kwenye kituo chochote cha Afya au hospitali ili waweze kupatiwa chanjo hiyo itakayowaweka salama dhidi ya kansa.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.