Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Eng.Andrea M. Kundo alipofanya ziara Wilaya ya Same jimbo la Same Mashariki katika kata ya Vuje na Bombo leo tarehe 17/07/2021.Eng.Kundo ameambatana na wataalamu wa taasisi mbalimbali ambao ni TCRA,UCSAF,meneja wa TTCL mkoa,meneja wa Posta mkoa na watoa huduma wa makampuni ya simu kama Tigo,Vodacom na Halotel ili wasikilize kero za wananchi na kutoa majibu jinsi gani wanazifanyia kazi mapema .Wananchi wa jimbo mla Same Mashariki wametoa shukrani zao za dhati kwa Mbunge wa jimbo hilo Mhe.Anna Kilango Malechela kwa kumleta Mhe.Andrea M. Kundo kusikiliza kero zao za mawasiliano ambapo zimedumu kwa muda mrefu.
Akijibu kero za wananchi Eng.Kundo alimtaka mtaalamu wa TCRA Eng.Imelda kujibu swali linalohusiana na redio ya Tanzania kupatikana Same ambapo Mhandisi huyo amesema masafa ya wilaya ya Same yameshatengwa na yatatangazwa ndani ya mwezi wa 7 ili wananchi na taasisi ndani ya wilaya ya Same wafanye maombi.
Hali kadhalika mtaalamu wa UCSAF ameagizwa kushirikiana na watoa huduma wa makampuni ya Tigo,Vodacom na Halotel ili kuhakikisha minara inafanya kazi na minara itakayojengwa ianze na 3G ili wananchi wapate mawasiliano.
Eng.Kundo amesema Serikali imetenga bajeti ya kuweka minara ya mawasiliano katika kijiji cha bwambo,mweteni na vugwama.
Mhe.Kundo ameagiza ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kukutana na watoa huduma ndani ya wilaya kabla ya kuwekeza katika maeneo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Same aagizwa kushiriki kutoa tathimini ya eneo na gharama zake.
Aidha mbunge wa Same Masharaki Mhe.Anna Kilango Malechela amesema jimbo hilo limepokea fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara ambapo mkandarasi ataanza kazi mara moja.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.