Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi kwa kuwaacha mbali wagombea wengine katika uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika kwenye Kata mbili Wilayani Same Julai 13 mwaka huu.
Kata zilizoshiriki uchaguzi wa marudio ni Kata za Njoro na Kalemawe mbapo katika Kata ya Njoro Mgombea wa CCM Comred Omar Abdallah ameshinda baada ya kupata kura 981 akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa NCCR -Mageuzi Bw.Raphael Mrutu aliyepata kura 69.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kwenye Kata hiyo Benedict Lopa alisema Mgombea Rashid Msuya wa ADC alipata kura 8 na wa mwisho ni Paulo Mshana wa TLP aliyepata kura 6.
Msimamizi huyo alimtangaza Omar Abdallah wa CCM kuwa Diwani wa Kata ya Njoro.
"Jumla ya wapigakura 2495 walijiandikisha kupiga kura na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 1070 ambapo kura halali zilikuwa 1064 na kura 6 zilikataliwa"alifafanua Lopa.
Kwenye Kata ya Kalemawe aliyekuwa mgombea wa CCM Comred Jofrey Jofrey alishinda kwa kura 1489 akifuatiwa na mgombea Helena Juma wa TLP aliyepata kura 107 ambapo mgombea Musa Philipo wa CUF alipata kura 50.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika Kata ya Kalemawe, Christopher Mteri alisema wapigakura walioandikishwa walikuwa 2506 huku waliopiga kura wakiwa 1648 ambapo kura 2 ziliharibika.
Msimamizi huyo alimtangaza Jofrey Jofrey wa CCM kuwa ndiye Diwani wa Kata ya Kalemawe.
Msimamizi wa Uchaguzi katika majimbo ya Same Mashariki na Same Magharibi Bi.Anastazia Tutuba alisema zoezi zima la Uchaguzi lilikuwa la Amani na utulivu na uchaguzi ulikuwa huru na haki.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.