Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Same Bi.Hamisa Chacha ameiomba Serikali kuiongezea Wilaya ya Same kiasi cha fedha zinazokadiriwa kwaajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kutokana na jiongrafia ya milima na miamba katika Wilaya hiyo ambayo inaongeza gharama ya ujenzi.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani katibu huyo amesema makadirio ya ujenzi yanayofanywa na Wizara wakati mwingine lyanaleta changamoto katika utekelezaji wa Miradi kwani fedha zinakuwa hazitoshi.
“Serikali inaleta fedha za kujenga darasa moja kwa shilingi milioni ishirini hadi ishirini na tano pamoja na kuweka madawati,fedha hii katika maeneo yetu ni ngumu sana kukamilisha darasa kutokana na jiografia ya huku” amesema Bi.Hamisa
Amesema katika sehemu nyingi ambazo Miradi inatekelezwa katika Wilaya ya Same wahusika wanalazimika kusafiri umbali usiopungua kilomita 70 kufuata vifaa vya ujenzi ambapo wakati mwingine hata gari haiwezi kufika katika eneo la ujenzi hivyo kulazimika kutumia vibarua kubeba na kuvifikisha site.
Bi.Hamisa amesema katika kusafirisha vifaa tuu tayari makisio ya bajeti yanaanza kuleta shida maana bajeti ilivyotengenezwa haikukadiria umbali wa kusafirisha vifaa wala haijakadiria gharama za kukata mlima na kusawazisha ili kupata eneo la ujenzi.
“Niiombe Serikali isitukadirie bajeti ya ujenzi wa darasa sawa na wakazi wa Kinondoni au maeneo mengine ya tambarare maana jiografia yetu ni ngumu na waje watembelee kujionea” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anastazia Tutuba amesema gharama za ujenzi katika maeneo ya milimani ni kuwa na tayari wameshaomba Serikali kuwaongezea fedha ili Miradi iweze kukamilika.
“Tuliomba kuongezewa fedha za miradi kutokana na jiografia yetu na zimeongezwa lakini ndo tumeambiwa tulaze tofali na ukilaza tofali zinaenda nyingi hivyo kunakuwa hakuna nafuu,tunajazia fedha za mapato ya ndani ili Miradi ikamilike lakini Miradi ni mingi hatuwezi kuikamilisha yote kwa mapato ya ndani” amesema Anastazia
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.