Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mhe.Christopher M.Irira ameendesha kikao cha kawaida cha baraza la madiwani leo tarehe 31 Agosti 2018 kilichojadili na kupokea mihtasari ya kamati za kudumu za Halmashauri,taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Same na maamuzi mbalimbali juu ya watumishi wa halmashauri na diwani.
Mhe.Irira amewawataka waheshimiwa madiwani kutambua kuwa suala la kuhamasisha wananchi katika masuala mbalimbali ya maendeleo ni jukumu la madiwani bila kujali itikadi za kisiasa kwani maendeleo ni kwa ajili ya watu wote .Aidha Mhe.Irira ametoa adhabu kwa kumsitishia diwani wa bendera kutokuingia kwenye vikao vitatu ikiwa ni maamuzi yaliyoazimiwa na kamati ya nidhamu ya madiwani kutokana na kosa la kuanzisha vurugu na kuwarushia mawe wasimamizi wa uchaguzi mdogo uliofanyika kata ya Makanya.
Sambamba na hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija amejibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waheshimiwa madiwani yakiwemo maswali ya papo kwa hapo yanayohusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Same.
Hatua mbalimbali zachukuliwa dhidi ya watumishi ikiwemo kumthibitisha Mhandisi wa maji kuwa mkuu wa idara ya Maji Eng.Musa Msangi na watumishi watendaji kata wawili(2) waliokuwa na kesi wafukuzwa kazi.
Pamoja na matukio hayo katika Baraza hili kulikuwa na tukio la kumuapisha diwani wa kata ya Makanya Mhe.Ismail ambaye aligombea baada ya diwani wa kata hiyo aliyekuwa diwani wa CHADEMA kujiuzulu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.