Baraza la Biashara wilayani Same lahuishwa ambapo mgeni rasmi ni Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Senyamule ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo na Katibu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same.Wadau mbalimbali washirikishwa kama TANAPA,mashirika binafsi,wakulima,Wafanyabiashara,TCCIA,mwakilishi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara wote hao wakiwa ni wajumbe wa Baraza hilo.
Akizungumza katika kikao cha Baraza hilo Mhe.Rosemary Senyamule asisitiza wajumbe kuboresha kwa Blue Print,kuboresha kwa fursa mbalimbali za kibiashara na kutatua kero mbalimbali za kibiashara.Vilevile kufungua ukurasa mkubwa wa mapinduzi ya kibiashara wilayani Same ili wananchi wahamasike na kupata huduma bora zaidi.
Vikosi kazi mbalimbali ambavyo ni utalii,biashara,mazingira,kilimo,ufugaji na uvuvi,afya na elimu vyaundwa ili kuchochea utendaji mzuri wa Baraza hilo kwa manufaa ya wananchi.
Mhe.Senyamule aagiza Halmashauri na TANESCO kukaa vizuri na kujitathmini wapi wanakwama,ni kero gani zinajitokeza katika biashara ili kutatua na kuondoa kero hizo kwa wananchi na kuongeza mapato ya Wilaya ya Same kutokana na kuboresha huduma mbalimbali.
Vilevile Mkurugenzi Mtendaji aagizwa kushirikiana na wataalamu kuboresha na kubadili mtazamo na kufanya kazi kwa weledi ili wananchi wapate huduma nzuri na bora zaidi.
Awapongeza wanawake kupatiwa eneo kwa ajili ya usindikaji wa bidhaa mbalimbali kama wine katika kata ya Saweni.
Awashukuru Wizara ya Viwanda na Biashara kushiriki katika Baraza hilo.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.