Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu amesema Serikali ina mpango wa kujenga kwa lami Barabara zote zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani humo ili kupunguza adha ya ukarabati wa mara kwa mara kila mvua inaponyesha.
Mheshimiwa Babu ameyasema hayo wakati alipotembelea Barabara ya Mwembe -Mbaga-Myamba (Km 91) kukagua ukarabati wake baada ya Barabara hiyo kuharibiwa na Mvua za Elnino na kushindwa kutumika kwa zaidi ya wiki moja.
"Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa Barabara hizi zinajengwa kwa lami ili kuziimarisha zisiharibiwe na mvua mara kwa mara maana ukarabati wa mara kwa mara unaigharimu sana Serikali "alisema Mkuu huyo.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwaonya wananchi wanaotumia vyombo vya moto kutovuka madaraja pale wanapoona maji yamefunika daraja maana mvua za Elnino zimesababisha vifo vya watu watatu.
Akizungumza katika ziara hiyo Meneja wa TANROAD mkoani Kilimanjaro, Mhandisi Motta Kyando alisema zoezi la ukarabati wa madaraja na Barabara zilizoharibiwa na mvua unaendelea.
Meneja huyo alisema kwa upande wa Daraja la Hedaru linatarajiwa kujengwa upya maana lililopo ni dogo na Halima uwezo wa kupitisha maji na magogo yanayotoka milimani.
"Hili darajani dogo na ndio maana lilizibwa na magogo na kusababisha maji kusambaa kwenye makazi ya watu na kusababisha mafuriko,hivyo tunasubiri Elnino iishe ili tuijenge Daraja kubwa"alisema Mhandisi Motta.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alitembelea madaraja ya Hedaru,Makanya na Bangalala ambayo kingo zake ziliharibiwa na Mvua,pia alitembelea Barabara ya Mwembe -Mbaga-Myamba ambayo inakarabatiwa.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.