Bw.Nandi Rupia ni Afisa nyuki mstaafu kutoka Wilaya ya Same ambaye ameamua kujishughulisha na ufugaji wa nyuki kibiashara ambapo pia anatumia mazao ya nyuki katika kutibu maradhi mbalimbali ya binadamu.
Akizungumza kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya kaskazini yanayofanyika kwenye viwanja vya Themi Mkoani Arusha Bw. Rupia amesema utumiaji wa asali angalau kijiko kimoja kwa siku huimarisha afya ya mlaji na kumlinda na maradhi mbalimbali.
“Asali pia ni dawa ya kidonda, kuna wateja wengi nimewauzia asali ambazo walitumia kutibu vidonda vya nje na ndani ya mwili na imewasaidia wamepona” alisema Rupia.
Alisema kwa upande wa asali ya masega (asali ambayo haijachujwa) husaidia kuondoa tatizo la harufu mbaya mdomoni na kuimarisha afya ya mwili.
Kwa upande wa matumizi ya nta Bw.Rupia anasema kuwa nta hutumika kutengenezea mishumaa lakini pia hutumika kutengeneza mapambo na kutengeza vifungashio vya dawa.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.