Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda J. Mgeni,amekabidhi andiko la uendeshaji wa Tamasha la Same Utalii Festival (SUF) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw.Nkoba Mabula
Andiko hilo lina lengo la kutangaza na kukuza Utalii kwenye Wilaya ya Same ili kuweza kuinua Uchumi wa Wilaya ya Same.
Mheshimiwa Mgeni alisema utalii si tu fursa ya kiuchumi, bali pia njia ya kuboresha maisha ya wananchi na kuhifadhi mazingira na kufurahia rasilimali zilizopo hapa nchini.
“Wilaya yetu ya Same imezungukwa na hifadhi mbalimbali na vivutio vingine vya asili kama maporomoko ya maji na Mipango"alisema
Alisema Tamasha la Same Utalii Festival ambalo liliana rasmi mwaka huu litakuwa endelevu na litafanyika kila mwaka.
Aliongeza kuwa tamasha hilo ni jukwaa muhimu la kuhamasisha jamii kuhusu faida za uhifadhi na jinsi unavyoweza kuchangia katika ustawi wa kiuchumi.
Mgeni alitoa shukrani kwa Rais kwa kuendelea kutekeleza sera za maendeleo ya utalii, akieleza kuwa Wilaya ya Same ina vivutio vingi ambavyo havijatangazwa.
"Tumeona ongezeko la wageni, na kampuni tano tayari zimejitokeza kusafirisha watalii baada ya kuona muitikio wa watu kwenye tamasha la kwanza,” aliongeza, akionyesha matumaini makubwa kuhusu maendeleo ya utalii katika wilaya hiyo.
Kwa upande wake wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Nkoba Mabula, alisisitiza umuhimu wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo wilayani humo.
"Nimekuja kuona baadhi ya vivutio vyetu,nchi hii imebarikiwa, lakini tunahitaji orodha ya vivutio ili tuweze kufanya kazi zaidi ya kuvitangaza,” alisema.
Mabula alitaja umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na wananchi katika matumizi ya rasilimali za misitu, mashamba, na hifadhi ili kuongeza mapato.
Aidha, aliupongeza uongozi wa wilaya kwa kufanikisha tamasha la utalii, lakini alisisitiza umuhimu wa kuwa na vituo vya taarifa za utalii kila Wilaya.
Aliongeza kuwa, Wizara iko tayari kutoa ushirikiano kufanikisha tamasha hilo, akiamini litakuwa fursa ya kuimarisha utamaduni wa Wapare na kuwahamasisha wawekezaji kuzingatia mila na desturi za eneo. “Tunataka fedha zinazopatikana kutokana na utalii zibaki hapa Same,” alisisitiza.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.