Upimaji wa Ardhi Wilaya Same
UTANGULIZI:
Upimaji na Ramani ni kitengo katika Idara ya Mipango Miji chenye jukumu la kupima ardhi pamoja na utayarishaji wa ramani (Survey plan) mbalimbali za mjini na vijijini. Ramani hizo ni msingi wa kubuni, kutekeleza na kuratibu mipango ya maendeleo juu ya ardhi katika sekta na kwa matumizi mbalimbali.
UPIMAJI (Cadastral Surveys):
Upimaji ni uwekaji wa kumbukumbu za kiwanja, mahali kilipo na ukubwa wake. Kumbukumbu hizi zinahifadhiwa ,kimchoro kwenye ramani (survey plan), kimahesabu (Co-ordinates) na kuweka alama za mipaka (beacons) kwenye kiwanja husika na kuidhinishwa,kusajiliwa na Wizara ya Ardhi nyumba na makazi.
KAZI ZA MPIMAJI (Surveyor):
•Kazi za mpima ardhi zinajumuisha; kuweka mipaka ya viwanja vipya.
•Kurudishia mipaka ya viwanja ambavyo vimeshapimwa na mipaka yake(beacons) zimepotea
•Kuchora ramani za Kiwanja/Viwanja.
TARATIBU ZA UPIMAJI
Ardhi ni eneo la juu la uso wa dunia. Ardhi hii ni mali ya Serikali na msimamizi wake Mkuu ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ili mwananchi aweze kupewa hati Miliki ya kiwanja (ardhi), anatakiwa awe na muhtasari wa Kamati ya Maendeleo ya Kata unaodhibitisha uhalali wa ardhi hiyo.
Maombi ya kupimiwa ardhi yanatumwa kwa Afisa Ardhi wa Wilaya Same. Afisa Ardhi atafanya yafuatayo:-
•Kukagua eneo kuwa ni huru, halina mgogogro wa mipaka, halijawekwa rehani,
•Ardhi husika ina mchoro wa Mipango Miji ulioidhinishwa na Wizara ya Ardhi nyumba na makazi (Approved town Plan drawing)
•Ardhi husika haina upimaji uliokwisha fanyika kwa lengo la umilikishwaji ardhi.
Baada ya Afisa Ardhi kukamilisha ukaguzi wake, mpima wa Wilaya atatoa maelekezo ya upimaji (Survey Instruction) kwa mpimaji yeyote atakayehusika na zoezi la upimaji.
Baada ya upimaji kukamilika, nyaraka zote huwakilishwa kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kukaguliwa, kuthibitishwa na kusajiliwa kama kumbukumbu rasmi ya mipaka husika
Ili mwananchi aweze kupewa hati miliki ardhi Wilaya Same hana budi kuwa na kumbukumbu ya mipaka ya ardhi hiyo mahali ilipo na ukubwa wake. Pia anatakiwa awe na muhtasari wa Kamati ya Maendeleo ya Kata uliosaniwa na viongozi wahausika,kwa anayemiliki ardhi hiyo kimila au kwa aliyenunua ili kuthibitisha mmiliki wa ardhi hiyo kisheria.
Mwananchi huomba kupimiwa ardhi kwa lengo la kufanikisha umilikishwaji chini ya Sheria Sura Na. 390 (Sheria ya upimaji ardhi) na mchoro wa upimaji uliyoidhinishwa ndio uthibitisho rasmi wa mipaka ya ardhi iliyopimwa.
Faida za upimaji ni kama ifuatavyo:-
•Kuondoa tatizo la migogoro ya mipaka kwa kusuluhishwa kisheria.
•Kupata mikopo mbalimbali kwa kutumia raslimali ya ardhi iliyopimwa.
•Urasimishaji.
•Utambulisho wa mahali kiwanja kilipo.
•Kuongezeka dhamani ya kiwanja.
•Kupanga matumizi ya ardhi ili kuchangia maendeleo katika Wilaya yetu
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.