Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Elisha Mngwira amefanya ziara Wilayani Same ambapo amezungungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same na kutembelea katika kata ya Vudee kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa kata hiyo.Ziara hiyo ilikuwa ni pamoja na tukio la kumtambulisha Katibu Tawala Mkoa mpya Ndg.Kazungu ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za watumishi na hoja zilizojitokeza katika kamati ya bunge.
Hoja mojawapo iliyozungumziwa ni asilimia kumi(10) ya mapato ya halmashauri inayotolewa kwa walemavu,vijana na wanawake Mhe.Mngwira alisema Halmashauri inatakiwa kuonesha kiwango ambacho imetoa kwa kila hela inayokusanywa asilimia kumi yake itoke mara moja.Vikundi vinavyoleta maombi vinatakiwa vipitishwe kwenye WDC."Alisema Mhe.Mngwira"
Halmashauri ibuni vyanzo vipya vya mapato na ufwatiliaji wa karibu wa vyanzo vilivyopo na ufwatiliaji wa madeni sugu yanayodaiwa na Halmashauri.Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi itoe asilimia ya mapato kwa Halmashauri kwa kila geti."alisema Mkuu wa Mkoa".
Kuhakikisha Halmashauri inatumia mfumo wa kielektroniki wa kukusanyia mapato na usimamizi wa vifaa vinavyotumika kukusanyia mapato ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara wa mfumo wa kukusanyia mapato.
Kuimarisha menejimenti ya Halmashauri.
Kutoa taarifa za maendeleo ya mfuko wa jimbo ambapo taarifa ya matumizi ya mfuko kwa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri itolewe.
Uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi wote wahimizwe kushiriki zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa.
Utatuzi wa migogoro ya ardhi ambapo Halmashauri inatakiwa itenge maeneo mbalimbali kwa matumizi.
Mwisho Mhe.Anna Mngwira aliagiza maagizo yote aliyotoa kufanyiwa kazi ikiwemo Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha migogoro yote ya ardhi inamalizika.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.