Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la SAME MAGHARIBI NA MASHARIKI, kwa kuzingatia Kanuni ya 14 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka wa 2020 na kanuni ya 12 ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2020. Anakaribisha Maombi kwa Watanzania wenye Sifa na uwezo wa kujaza nafasi za Watendaji wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28.Oktoba, 2020 kama ifuatavyo:-
1. MSIMAMIZI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA (Nafasi 444)
2.WASIMAMIZI WASAIDIZI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA (Nafasi 888)
3. KARANI MWONGOZA WAPIGA KURA (Nafasi 444)
SIFA ZA MWOMBAJI KWA NAFASI YA MSIMAMIZI WA KITUO/WASIMAMIZI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA:-
I. Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi.
II. Asiwe shabiki au Kiongozi wa Chama Cha Siasa.
III. Awe mwadilifu elimu ya Kidato cha 4 au zaidi na anayeweza kusoma na kuandika vizuri. Pia anayeweza kuyaelewa maelekezo ya wasimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura.
IV. Ikiwezekana awe Mkazi wa Kata ambayo anaomba.
1. SIFA ZA MWOMBAJI KWA NAFASI YA KARANI MWONGOZA WAPIGA KURA.
I. Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi.
II. Awe Mkazi wa Kata ambayo atafanyakazi ya Kuongoza WAPIGA KURA.
Asiwe shabiki au Kiongozi wa Chama Cha Siasa.
III. Ikiwezekana awe Mpiga Kura wa Kituo anachofanya Kazi.
IV. Awe mwadilifu na mwenye Akili Timamu.
V. Awe na Elimu isiyopungua Kidato cha 4 na anayeweza kusoma na kuandika na kuyaelewa maelekezo ya Wasimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura.
IV. Asiwe shabiki au Kiongozi wa Chama Cha Siasa.
**MALIPO**
i.Malipo yatakuwa kama ifuatavyo:-
Msimamizi wa Kituo siku ya Uchaguzi atalipwa posho ya Tzs. 35,000 kwa siku kwa muda wa siku mbili, posho ya chakula Tzs 15,000 kwa siku moja na nauli Tzs 20,000;
ii. Msimamizi Msaidizi wa Kituo atalipwa posho ya Tzs. 30,000 kwa siku kwa muda wa siku mbili, posho ya chakula Tzs 15,000 na nauli Tzs 20,000; na
iii.Karani Mwongozaji Wapiga Kura atalipwa posho ya Tzs 30,000 kwa siku moja na posho ya chakula Tzs 15,000.
**MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE**
i. Waombaji waambatishe maelezo binafsi (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wawili.
ii. Maombi yote yaambatane na Vyeti vya taaluma, nakala za Vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita au kuhitimu mafunzo kwa kuzingatia sifa kwa mujibu wa Tangazo hili.
iii. Waombaji waambatishe picha mbili Passport size za hivi karibuni.
iv. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao.
iv.Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kugushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 27 Septemba , 2020.
Anuani ya kutuma maombi ya kazi ni:-
Msimamizi wa Uchaguzi,
Jimbo la Same Magharibi na Mashariki
S.L.P. 138
SAME.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.