Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndugu Christopher Michael Irira leo tarehe 10/06/2020 amevunja baraza la madiwani ikiwa ni kikao cha mwisho cha madiwani ambapo kamati mbalimbali za madiwani ambazo ni kamati ya fedha,uongozi na mipango,kamati ya uchumi,ujenzi na mazingira,kamati ya elimu afya na maji na kamati ya kudhibiti UKIMWI ziliwasilisha taarifa na shughuli mbalimbali zilizofanyika kwa kipindi chote.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi.Anna-Claire Shija aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Halmashauri ikiwa ni mradi ya ujenzi wa vituo vya afya,mradi wa vyumba vya madarasa mabweni na matundu ya vyoo,mradi wa ukamilishaji wa maboma pamoja na miradi ya maji.
Bi.Shija amewashukuru waheshimiwa madiwani na kipekee kabisa Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Irira kwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu na kufanya kazi kwa amani na utulivu bila migongano yoyote kwake pamoja na wataalamu wa Halmashauri ambao ni wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri.Bi.Shija amewatakia kila la heri waheshimiwa madiwani wanapoanza maandalizi ya kugombea nafasi za udiwani katika uchaguzi mkuu na kupata ushindi kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Mwisho kabisa Mhe.Irira amewatakia Mkurugenzi na wataalamu wa Halmashauri pamoja na watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Same kila la heri katika majukumu yao ya kila siku katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.