Tuesday 19th, March 2024
@Viwanja Vya Shule ya Sekondari Same
Siku ya uboreshaji na Ubadilishaji wa Mazingira ilifanyika Wilayani Same Tarehe 17Januari 2018 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Same.
Siku hiyo iliyoandaliwa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Mazingira wakiwemo FLORESTA,TSF,TANAPA Idara ya Maliasili na Wengine ilikuwa na Lengo la Kuelimisha na kuhamasisha wanajamii wote juu ya Upandaji wa Miti na Ujasiriamali ili kutokomeza Umasikini na Kubadilisha Mazingira Kuwa KIjani na kurudisha Edeni iliyoharibiwa kimazingira hatimaye kupata Mahusiano mazuri na kutegemeana kimaisha baina ya Viumbe hai (eco-System).
Shughuli zilizofanyika ni Upandaji Miti ambapo Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine wakiserikali,taasisi mbalimbali na wakidini Walishiriki katika zoezi la Upandaji wa Miti ikiwa ni Uzinduzi rasmi wa kupanda miti Eneo la Barabara ya Bomani kwa Umbali wa Km 2.
Shuguli za Ujasiriamali,Uzalishaji wa Viwanda vidogo,Kilimo,Misitu na Nyuki nazo zilipewa nafasi ya kufanya Maonyesho na Biashara za Bidhaa wanazo zalisha wadau wa na Wanachama wa Vikundi hivyo vya Uzalishaji. Siku hiyo pia ilitoa fursa kwa Vikundi vya VICOBA kushindanishwa na kutuzwa kwa washindi.
Kwa upande wa Burudani kulikuwa na Burudani za Asili ya Wapare maarufu kwa Kajanja,Kwaya ya Mamajusi kutoka Moshi na Ngonjera kwa Watoto wa Shule za Msingi.
Same ni Yetu na Same Itabadilika kwa Juhudi za kila Mtu anaehusika kwa Nafasi Yake.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.