Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg.Kheri James amewapongeza Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Same kwa kutekeleza majukumu yake vizuri na maagizo aliyowapa alipokuwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maagizo aliyotoa.Ndg.Kheri James amewataka UVCCM Same kuhamasisha na kuelimisha wananchi kwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2020."Dr.John Pombe Magufuli ni Rais wa kuigwa duniani"alisema ndugu Kheri James.
Ndg James ampongeza Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Senyamule,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija na CMT yake na Mbunge wa Same Mhe.David Mathayo David kwa kufanya kazi nzuri ya kuleta maendeleo kwa wana Same na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo itapelekea wananchi kukichagua Chama Cha Mapinduzi kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Octoba 2020.
Mwisho kabisa Ndg.Kheri James aliwaasa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuwalinda na kuwatia moyo watumishi wa serikali na kuwarekebisha pindi wanapokosea kwa kuwa watumishi wa serikali ndio watekelezaji na watendaji wakubwa wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.