Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Edward Jonas Mpogolo ameongoza maadhimisho ya siku ya Faru duniani ambapo yamefanyika Wilayani Same katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi Same leo tarehe 22/09/2021.Katika maadhimisho hayo Mhe.Mpogolo ameshukuru kwa kualikwa kuwa mgeni rasmi na kutoa pongezi za dhati kwa TANAPA,WWF na TFS kwa kuonesha uzalendo wa kulinda na kuhifadhi hifadhi ya Mkomazi.
Awaasa wana Same kutoa ushirikiano kwa TANAPA,WWF pamoja na wadau wengine.Vile vile ametoa wito kwa wana Same kuwekeza kwa kujenga hoteli za kitalii ili kupata mafanikio katika wilaya ya Same na kujiongezea kipato kwa mwananchi mmoja mmoja na Wilaya kwa ujumla.Mhe.Mpogolo amewaasa wana Same kufanya utalii katika hifadhi ya Mkomazi
Amewataka Menejimenti ya Halmashauri,watendaji wote wa Halmashauri,kamati ya ulinzi na usalama kufanya utalii katika hifadhi ya mkomazi.
Wanafunzi wa shule za sekondari waahidiwa kuandaliwa programu maalumu ya kwenda kuona wanyama kwa kuzingatia wanafunzi watanaofanya vizuri katika masomo.
Aidha Mwenyeki wa Halmashauri Mhe.Yusto Mapande amewasisitiza wana Same kuchangamkia fursa ya utalii kwa kufanya biashara na shughuli mbalimbali ili kujipatia kipato.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Same Bi.Anastazia Tutuba amewasisitiza pia wananchi wa same kuwekeza kwa kujenga hoteli za kitalii na biashara mbalimbali.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.