Wanafunzi Same sekondari wafanya mahafali ya kumaliza kidato cha sita kama skauti.
Wapongezwa kwa kushiriki matukio mengi ya serikali na jamii kwa kujitolea na kwa ubunifu mkubwa.Wanafunzi wengine waaswa kujiunga na skauti.
Viongozi wakumbushwa kutumia vizuri nafasi iliyotolewa na serikali kuhakikisha kila shule inakuwa na skauti na ikiwezekana wanafunzi wote wapitie mafunzo ya skauti.
"Mtu aliyepitia skauti atakuwa mzalendo,mbunifu,mchapakazi,jasiri,mkakamavu,mwaminifu,mcha Mungu na mwenye upendo.Kila Taifa ligependa kuwa na watu wenye sifa hizi.Na hii ndiyo sababu serikali imeagiza kila shule kuwe na skauti.Na Rais ndiye aliyeteua kiongozi wa skauti taifa".Alisema DC wa Same Mhe.Rosemary Senyamule aliyekuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo ambaye pia ni mlezi wa skauti Wilaya.
Ampongeza Bi.Stella Mongi kwa kuchaguliwa kuwa kamishna mpya wa skauti Wilaya.Amtaka kuongeza idadi ya wanachama wa skauti.
Awataka skauti kuonesha mafunzo yao kwa vitendo katika mitihani yao ya taifa na kokote wanakoenda.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.