Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Stacki Senyamule ameongoza maelfu ya wananchi wa Same katika zoezi la kupokea Mwenge wa Uhuru leo Juni 26 ,2019 kutoka Wilaya ya Mwanga uliokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Mwanga chini ya uangalizi wa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu,Mzee Mkongea Ali.
Mapokezi ya Mwenge wa uhuru yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Njoro vilivyopo ndani ya kata ya Njoro.
Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mwenge wa Uhuru 2019 umetembelea jumla ya miradi mitano yenye thamani ya Shil.1,059,125,337/=.Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa uliopo shule ya Makanya sekondari kata ya Makanya uliogharimu Shil.44,200,000/=, mradi wa ujenzi wa barabara ya bomani kata ya Stesheni uliogharimu Shil.429,501,000/=.,mradi wa wodi ya wanaume hospitali ya wilaya uliopo ndani ya kata ya Same uliogharimu Shil.98,304,443/=,mradi wa maji uliopo kata ya Mhezi uliogharimu Shil.388,177,012/= na mradi wavibanda vya biashara stendi uliopo kata ya Same uliogharimu Shil.98,942,882/=
Akizungumza wakati alipotembelea mradi wa maji kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu Mzee Mkongea Ali amekiri kuwa mradi huo ni mzuri na kwa kuwa utahudumia zaidi ya kaya 200 katika kata ya mhezi na kupunguza kero kubwa ya maji kwa wakazi wa kata ya Mhezi.
Sambamba na hayo Mwenge wa Uhuru umezindua klabu za kupinga rushwa zinazohusu wanafunzi wa chuo cha uuguzi kilichopo hospitali ya wilaya ya Same ndani ya kata ya Same ambapo kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu Mzee amezindua club hiyo pamoja na kuwakabidhi vyeti vijana hao.
Vijana hao walienda mbali zaidi wakionyesha kuelewa wanachokizungumza kwa kujibu maswali yote yahusuyo rushwa kutoka kwa ndugu Mzee,huku wakitoa misemo mbalimbali na kuitikia,”Rushwa ni adui wa haki”na “Kataa rushwa, jenga Tanzania”
Mhe. Senyamule ameitaka klabu hiyo kuwa chachu ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii za Same na kuahidi kuwa pamoja nao katika kuhakikisha kilichoanzishwa kinakuwa kwa mafanikio na malengo yaliyokusudiwa yanatimia. Hii ni sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya Mhe.John Pombe Magufuli inayopinga na kupambana vikali dhidi ya rushwa za aina zote nchini.
Aidha,Baada ya taarifa ya Wilaya na miradi iliyotembelewa,kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru Mhe.Senyamule amemkabidhi Mwenge huo wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Elisha Mngwira ili aukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mhe.Mkuu wa mkoa wa Tanga na kuanza mbio za Mwenge 2019 ndani ya mkoa wa Tanga.
Ndugu Mzee kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akizindua mradi wa barabara bomani kata ya Stesheni
Ndugu Mzee kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa akizindua mradi wa wodi ya wanaume hospitali ya wilaya Same
Ndugu Mzee kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa akizindua mradi wa vibanda vya biashara stendi
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.